Serikali ya China imefuta rasmi muswada uliowasilishwa nchini humo, wa kuwapeleka watuhumiwa kutoka katika kisiwa cha Hong Kong katika Bara ya China kushitakiwa, hali iliyosababisha maandamano makubwa katika kisiwa hicho.
Kwa zaidi ya miezi mitano, Wakazi wa kisiwa cha Hong Kong wamekuwa wakishiriki katika maandamano ya kupinga muswada huo, maandamano yaliyokuwa yakiambatana na ghasia, licha ya Serikali ya China kutangaza kuutupilia mbali.
Waandamanaji walikuwa wakidai kuwa, polisi walikuwa wakitumia nguvu kubwa kutawanya maandamano yao, na kwamba muswada huo ni sehemu ndogo ya madai yao kwa Serikali ya China.