Rais John Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi(ARU).
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa, Msuya ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi kingine cha miaka miwili.
Uteuzi huo umeanza Oktoba 22 mwaka huu.