Waasi 14 wauawa katika mapigano Burundi

0
781

Vikosi vya Serikali ya Burundi vimewaua Waasi 14 na kukamata bunduki 11, baada ya kuzuka kwa mapigano makali katika wilaya ya Musigasi.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Burundi imeeleza kuwa, Waasi waliouawa ni wa kikundi cha Red – Tabara ambacho kwa muda mrefu kimekua kikiupinga uongozi wa Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo.

Vikundi kadhaa vya Waasi ambavyo vimekua vikiipinga Serikali ya Rais Nkurunziza vilianzishwa mwaka 2015, baada ya kutokea kwa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.

Wakazi wa wilaya hiyo ya Musigasi wamekua wakiyakimbia makazi yao kwa hofu ya mapigano na kusema kuwa, Waasi hao wa Red – Tabara wamekua wakitokea katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Vikundi vya Waasi vya Red – Tabara, FNL – Nzabampema na Forebu ni miongoni mwa vikundi ambavyo vimekua vifanya uasi katika eneo la Mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na mara kadhaa vimekua vikivuka mpaka na kuingia nchini Burundi ambapo nako vimekua vikiendesha mapigano.