Chama cha wahasibu Tanzania -TAA kwa kushirikiana na wakuu wa mikoa
nchini wameandaa maonesho ya dawati la mhasibu yatakayofanyika Novemba
Pili mwaka huu katika kanda tano nchini.
Maonesho hayo yatakuwa na lengo la kutoa huduma za kitaalamu bila
malipo kwa wafanyabiashara wa kampuni za bima, benki na washauri wa
kodi.
Akizungumza jijini Dar Es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa chama cha
wahasibu Tanzania Odemari Rushita, amesema kwa kanda ya Kaskazini
maonesho hayo yatafanyika Kilimanjaro, Kanda ya ziwa Mwanza, Kanda ya
kati Dodoma, Kanda ya Kusini Mbeya na Kanda ya Mashariki Dar Es
Salaam.