Mauzo ya hisa DSE yapanda

0
3161

Mauzo ya hisa katika soko la hisa la Dar Es Salaam -DSE yamepanda
kutoka hisa Milioni 1.06 kufikia hisa milioni 3.62 wiki hii.

Mauzo hayo yanatajwa kuchangiwa zaidi na wawekezaji wa ndani ambao
walichangia asilimia 99 ya thamani ya manunuzi yote huku wawekezaji wa
nje wakichangia kwa asilimia 56.25.

Afisa Miradi wa soko hilo, Emmanuel Nyalali amesema kuwa Kaunta ya
CRDB ndio ilioongoza kwa kuchangia asilimia 75.22 ya mauzo ikifuatiwa
na Twiga kwa asilimia 15.94 na TBL kwa asilimia 5.33.