Bodi ya Bonde la Wami Ruvu imewataka wadaiwa sugu wenye visima kwa
matumizi ya biashara kulipa tozo wanazodaiwa kwa wakati kabla ya
sheria kuchukua mkondo wake.
Hayo yamesemwa na Afisa Maji wa Bodi ya Bonde la Wami Ruvu, Simon
Ngonyani jijini Dar Es Salaam na kufafanua kuwa katazo la Waziri wa
Maji liliwalenga wenye visima kwa matumizi ya nyumbani na si
wenye visima vya biashara.
Amesema kufutwa kwa tozo hizo hakumaanishi kwamba wachimbaji wa
visima hawataomba vibali.
Zaidi ya shilingi milioni 328 zinadaiwa na Bodi ya Maji ya Bonde la
Wami Ruvu kwa watumiaji wa maji ya visima kwa matumizi ya biashara.