Waziri Hasunga azindua vitabu vya kahawa

0
155

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema miongoni mwa changamoto za kuimarisha ubora wa kahawa ni uzalishaji mdogo wa miche ya zao hilo
huku mahitaji yakiwa ni makubwa kwa wakulima.

Akizungumza katika uzinduzi wa vitabu vya kanuni bora na mitaala ya
ufundishaji wa zao hilo mkoani Kilimanjaro Waziri Hasunga amesema ili
kukabiliana na changamoto hiyo serikali inakusudia kuzalisha mbegu
bora za kahawa kwa lengo la kubadilisha mikahawa ya zamani ipatayo
milioni 240 kwa kutumia aina mpya za kahawa.

Waziri Hasunga amesema uzalishaji wa miche milioni saba kwa mwaka ni
kidogo, ambayo itachukua takribani miaka 35 kubadili aina ya zamani
hivyo amesema serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo
itahakikisha kunakuwa na mapinduzi ya kilimo cha kahawa nchini.