JPM Awapa NENO Wateule Wake

0
353

Rais John Magufuli amewataka Viongozi mbalimbali ambao amekua akiwateua, kufanya kazi kwa weledi, kuwatetea pamoja na kuwatumia Wananchi Wanyonge.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo Ikulu  jijini Dar es salaama, wakati wa hafla ya kuwaapisha Viongozi
mbalimbali aliowateua  hivi karibuni.

“Kazi hizi ni lazima tuwatumikie Wananchi, juzi nilikuwa Mtwara, tulikuta malalamiko ya Wakulima wa korosho ambao wamedhurumiwa malipo yao tangu msimu wa 2016/2017 na tulijua ni Vyama Vya Ushirika Kumi, baada ya kumuagiza Brigedia Jenerali wa TAKUKURU wamebaini ni vyama 32 ambavyo vimewadhulumu watu hao takribani Shilingi Bilioni 1.2 na tayari viongozi 99 wameshashikwa na wamesharudisha Milioni 255, na Brigedia Jenerali amenihakikishia lazima zilizobaki waziteme”, amesema Rais Magufuli.

Amesisitiza kuwa Kiongozi yeyote anayemteua ni lazima akawatumikie Wananchi bila uonevu na kamwe asiogope kuchafuliwa kwa kuwa kuchafuliwa katika uongozi ni jambo la kawaida.

Pia amewataka Viongozi hao kuwa Wavumilivu na kumtanguliza Mwenyezi Mungu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Viongozi walioapishwa hii leo ni Mathias Kabunduguru anayekua Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Godfrey Mweli anayekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja Ali Sakila Bujika anayekuwa Balozi.