Bodi ya Wakala wa Huduma za Vivuko nchini Kenya yavunjwa

0
254

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, ametengua uteuzi wa Wajumbe Watano wa Bodi ya Wakala wa Huduma za Vivuko nchini humo, zikiwa zimepita takribani wiki Tatu baada ya kutokea ajali ya kuzama mama na mtoto wake katika eneo la Likoni.

Katika tukio hilo lililotokea mwezi Septemba mwaka huu, Mariam Kighenda na mtoto wake Amanda Mutheu walifariki dunia baada ya gari waliokua wamepanda lililokua ndani ya kivuko cha MV Harambee kuteleza na kutumbukia baharini.

Tangu kutokea kwa ajali hiyo, baadhi ya Wananchi wa Kenya wamekua wakiishutumu Serikali kwa kusema kuwa imezembea katika suala la uokoaji na kusababisha miili ya watu hao kupatikana baada ya siku 13, hivyo kutaka wahusika wote wawajibishwe.

Miili ya Mariam na mtoto wake iliopolewa baharini na Kikosi cha Wazamiaji kutoka nchini Afrika Kusini baada ya Wazamiaji wa Kenya kushindwa kufanya kazi hiyo.