Waziri Mkuu akemea ujenzi mbovu wa kuta, aagiza zibomolewe

0
232

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameeleza kutoridhishwa na ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi hasa katika baadhi ya majengo na kumuagiza Mhandisi wa halmashauri ya wilaya hiyo,- Tengamaso Wilson abomoe kuta zenye hitilafu na kurekebisha kasoro zilizopo kwenye majengo hayo.

https://www.youtube.com/watch?v=lb051pu9F7g&feature=youtu.be

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akikagua majengo ya hospitali hiyo, ambapo miongoni mwa majengo aliyoyakagua na kutoridhishwa na ujenzi wake ni la Utawala, Wagonjwa wa nje (OPD) pamoja na lile la maabara.

“Kuta zimepishana unene kwa sababu hukusimamia kazi yako ipasavyo, ukuta huu ni mbovu kwa sababu hukuwasimamia vizuri mafundi wako, kuna mahali juu unaona ukuta ni mdogo na huku chini ni mnene, Mhandisi wa wilaya simamia hili, kagonge upya kuta za jengo hili na lile, hatuwezi kuwa na jengo la Serikali la aina hii, tukitoa fedha ya Serikali ni lazima mjiridhishe kama kilichojengwa ndicho sahihiā€, amesema Waziri Mkuu.