Watu Tisa wamethibitika kuuawa nchini Guinea, baada ya kutokea kwa maandamano ya Raia wa nchi hiyo, wanaopinga Rais Alpha Conde kugombea kiti hicho kwa muhula wa Tatu.
Rais Conde mwenye umri wa miaka 81 aliingia madarakani mwaka 2010, na kipindi chake cha mwisho cha uongozi kinamalizika mwaka 2020.
Kumekua na taarifa nchini Guinea zinazoeleza kuwa, Rais Conde ana mpango wa kubadilisha katiba ya nchi hiyo ili aweze kugombea kwa muhula wa Tatu, hali iliyozusha maandamano.
Rais Conde mwenyewe amesema kuwa, hana mpango wa kugombea nafasi hiyo kwa muhula wa Tatu, lakini kitendo chake cha kutaka kufanya mabadiliko ya Katiba ya Guinea kimetafsiriwa kuwa ana nia ya kuwania tena kiti cha Urais.