AS Roma nayo kutumia Kiswahili

0
985

Klabu kubwa ya Mpira wa Miguu ya AS Roma ya nchini Italia, imezindua akaunti mpya katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwa lugha ya Kiswahili

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Klabu hiyo, -Paul Rogers amesema kuwa AS Roma imeamua kufungua akaunti hiyo ili iweze kuwafikia Wapenzi na Mashabiki wengi zaidi katika nchi zilizopo katika eneo la Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na Kusini mwa Afrika.

AS Roma imefungua akaunti hiyo kwa lugha ya Kiswahili zikiwa zimepita siku chache baada kutumia akaunti yake nyingine ya lugha ya Kiingereza kumpongeza mwanariadha wa Kenya- Eliud Kipchoge baada ya kuweka rekodi katika historia ya mbio za Marathon, ambapo ilitumia lugha ya Kiswahili.

Baada ya kupostiwa kwa pongezi hizo kwa lugha hiyo ya Kiswahili, yalitolewa maoni lukuki kutoka kwa Wapenzi na Mashabiki waliopo kwenye nchi zinazotumia lugha ya Kiswahili, ambao pia waliomba kuwepo kwa akaunti ya aina hiyo, jambo ambalo limetekelezwa haraka.