Serikali yashinda kesi, Wakurugenzi kuendelea kusimamia uchaguzi

0
247

Serikali imeshinda Rufaa dhidi ya kesi iliyofunguliwa na Bob Wangwe kupinga Wakurugenzi Kusimamia uchaguzi.

Mahakama ya Rufani Tanzania imetengua hukumu na amri ya Mahakama Kuu kuzuia Wakurugenzi wa Halmashauri, Manispaa na Majiji nchini kusimamia uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Mahakama ya Rufani imefikia uamuzi huo hii leo baada ya kujiridhisha na hoja za Serikali kuwa Wakurugenzi hao kabla ya kuwa Wasimamizi wa uchaguzi, hula viapo vya kukana uanachama wao.