Wambura kuongoza Idara ya Habari na Masoko TFF

0
975

Boniface Wambura ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF) baada ya kumaliza mkataba wake wa kuitumikia nafasi ya Afisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi (TPLB).

Katika nafasi hiyo mpya, Wambura atakua akisaidiwa na Cliford Ndimbo atakayeshughulikia Habari pamoja na Aron Nyanda atakayeshughulikia Masoko.

Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao amewaeleza Waandishi wa habari kuwa, nafasi ya Afisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi iliyokuwa ikishikiliwa na Wambura itatangazwa katika siku zijazo.

Kidao ameongeza kuwa, Kamati ya Utendaji ya TFF pia imemthibitisha Oscar Mirambo kuwa Mkurugenzi wa Ufundi ambapo awali alikuwa akikaimu nafasi hiyo.