Rais atoa Shilingi Milioni 10 kwa shule ya Viziwi Lukuledi

0
179

Rais John Magufuli ametoa Shilingi Milioni Kumi kwa shule ya Sekondari ya Viziwi Lukuledi, ili isaidie kumaliza matatizo mbalimbali yanayowakabili wanafunzi hao.

Akihutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Lukuledi wilayani Masasi mkoani Mtwara, Rais Magufuli amesema kuwa anafahamu kero za wanafunzi hao na ametoa fedha hizo ili ziwasaidie.

Rais Magufuli ametoa fedha hizo baada ya kupata maelezo kutoka kwa Mwalimu Emmanuel Msamila anayewasimamia Wanafunzi hao, ambapo pia ameahidi kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kuisaidia shule hiyo ya Sekondari ya Viziwi Lukuledi.

“Nimefurahi sana kuwaona wanafunzi wenye matatizo ya kusikia na hapa naomba kuwachangia Shilingi Milioni 10 hapahapa ili mkatatue shida zenu, hizo shida nyingine nitazungumza na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako ili tuyamalize”, amesisitiza Rais Magufuli

Rais Magufuli ameanza ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara, ambapo mbali na kuzungumza na Wakazi wa mkoa huo pia anakagua miradi mbalimbali ya maendeleo.