TFF yatangaza mabadiliko ya Katiba

0
169

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza mabadiliko ya Katiba ya shirikisho hilo, ambayo pamoja na mambo mengine yanahusu mfumo wa uongozi.

Mabadiliko hayo yametangazwa na Katibu Mkuu wa TFF, -Wilfred Kidao ambapo kwa mujibu wa mabadiliko hayo nafasi ya Makamu wa Rais kuanzia sasa haitakua ya kuchaguliwa kwa kupigiwa kura, bali itakuwa ni ya kuteuliwa na Rais wa Shirikisho hilo.

Mabadiliko mengine ni katika idadi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ambayo kwa sasa itapungua kutoka 22 hadi 13 na Kanda kupunguzwa kutoka 13 hadi kufikia Sita.

Katika mabadiliko mengine, Wajumbe wa mkutano mkuu watapungua kutoka 129 hadi kufikia 87, hatua inayomaanisha kuwa kila mkoa katika mikoa 26 ya Tanzania Bara utatoa wajumbe
Wawili, Wajumbe 20 watatoka kwenye vilabu na vyama washirika vitatoa Wajumbe 15.