TMA yatoa tahadhari ya kunyesha kwa mvua kubwa

0
201

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa kati ya kesho tarehe 17 na tarehe 18 mwezi huu katika baadhi ya maeneo nchini.

Kwa mujibu wa TMA, maeneo yatakayopata mvua hizo ni ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini ambayo ni mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.

“Uwezekano wa mvua kutokea ni wastani na kiwango cha athari na baadhi ya makazi yatazungukwa na maji mengi, hivyo ni muhimu kwa Wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari”, imesema taarifa ya TMA.