Kipchoge arejea Kenya baada ya kuweka rekodi Marathon

0
921

Mwanariadha wa Kenya, – Eliud Kipchoge amerejea nchini Kenya leo hii akitokea nchini Austria,  ambapo ameweka rekodi katika historia ya mbio za marathon kwa kuwa mtu wa kwanza kukimbia Kilomita 42 kwa muda wa chini ya saa mbili.

Wafanyakazi mbalimbali wa Shirika la Ndege la Kenya, wameposti picha katika mitandao ya kijamii wakiwa na Kipchoge, alipokua akikwea pipa katika uwanja wa ndege wa Amsterdam nchini Uholanzi.

Katika shindano la Ineos lililofanyika mjini Vienna  Jumamosi iliyopita, Kipchoge  alikimbia Kilomita 42.2 katika muda wa saa Moja, dakika 59 na Sekunde 40.

Mwanariadha huyo ambaye ni Bingwa wa Olimpiki, alikuwa ameikosa rekodi
hiyo kwa  sekunde 25 katika jaribio lake la mwaka  2017 na pia ni bingwa  mara Nne wa London Marathon.