Waliowadhulumu Wakulima wa Ufuta kuwajibishwa

0
163

Rais John Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwawajibisha watu wote ambao wamekua wakiwadhulumu Wakulima wa ufuta katika jimbo la Ruangwa mkoani Lindi na maeneo mengine nchini.

Rais Magufuli pia amemuagiza Naibu Waziri wa Kilimo Hussen Bashe na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) Brigedia Jenerali John Mbungo kubaki wilayani Ruangwa ili kushughulikia suala la Vyama Kumi vya Ushirika wa Wakulima vilivyoshindwa kuwarudishia Wakulima wa Ufuta fedha walizowadhulumu.

“Waziri Mkuu umekuwa mpole sana kwa wapiga kura wako halafu kwingine unatumbua tu, basi na hapa usiogope we tumbua tu, vifaa vya kutumbulia nimeishakupatia”, amesema Rais Magufuli.

“Nakuagiza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo ubakie hapa wewe na Naibu Waziri Bashe, mbaki hapa mshughulikie suala hili”. amesisitiza Rais Magufuli.

Wakulima wa ufuta wilayani Ruangwa wamedhulumiwa zaidi ya Shilingi Bilioni 419 na vyama vya Ushirika vya Wakulima wa Ufuta -AMCOS.