Rais Magufuli : Serikali imefanya mengi kumuenzi Nyerere

0
233


Rais John Magufuli amesema kuwa, Serikali ya awamu ya Tano imefanya mambo mengi katika kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nayerere ikiwa ni pamoja na kusimamia nidhamu Serikalini, kuyafufua Mashirika ya Umma, kurejesha nidhamu katika Utumishi wa Umma na kulinda Rasilimali za Taifa.


Akihutubia katika kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru zilizokwenda pamoja na Kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa na Kilele cha wiki ya Vijana Kitaifa kwenye uwanja wa Ilulu mkoani Lindi, Rais Magufuli amesema kuwa, Serikali pia imefufua Shirika la Usimamizi wa Huduma za Meli nchini, ili liendelee kuwahudumia Wananchi.


Amesema kuwa, jitihada zote hizo zimelenga katika kuziishi fikra za Baba wa Taifa ambaye alilijenga Taifa la Tanzania katika misingi ya Ujamaa na Kujitegemea na kuahidi kuwa misingi hiyo ndiyo itawafanya Watanzania kuwa huru siku zote.


Kwa mujibu wa Rais Magufuli, Serikali ya awamu ya Tano itaendelea kusimamia Rasilimali za Taifa ikiwa ni pamoja na k