Miradi 1, 390 yazinduliwa na Mwenge mwaka 2019

0
225

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema kuwa, jumla ya miradi 1, 390 yenye thamani ya Shilingi Trilioni 4.7 imezinduliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu katika maeneo mbalimbali nchini.

Akihutubia kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya miaka 20 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na maadhimisho ya wiki ya Vijana Kitaifa huko mkoani Lindi, Waziri Mhagama amesema kuwa, miradi mingine 107 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 90.2 imetiliwa shaka na hakizinduliwa wala kuwekewa mawe ya msingi na Mwenge wa Uhuru kutokana na kasoro mbalimbali zilizobainika katika miradi hiyo

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ile ya Maji, Barabara, Elimu na ujenzi wa majengo ya umma, ambayo ilibainika kutokuwa katika mpangilio ulikubaliwa wakati wa makubaliano.

Waziri Mhagama amesema kuwa, miradi iliyokataliwa na mwenge wa Uhuru ipo katika Halmashauri 82 Tanzania Bara na Zanzibar, na kwamba miradi hiyo ilikosa ulinganifu wa thamani ya fedha na uhalisia wa miradi yenyewe.