Makonda aridhishwa na kasi ya ujenzi wa Machinjio

0
169

Kufuatia agizo la Rais John Magufuli alipotembelea ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti yaliyopo jijini Dar es salaam na kutaka ujenzi huo uwe umekamilika ndani ya muda wa miezi mitatu, ujenzi huo unaendelea vizuri.


Tangu kutolewa kwa agizo hilo, uongozi wa mkoa wa Dar es salaam ukiongozwa na Mkuu wa mkoa huo Paul Makonda, umekua ukisimamia ujenzi wa machinjio hayo usiku na mchana ili kuhakikisha unakamilika ndani ya muda uliotolewa na Rais.


Makonda ameelezea kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo na kuongeza kuwa, ni matumaini yake utakamilika ndani ya muda huo wa miezi mitatu uliotolewa na Rais Magufuli.