Serikali imetangaza kuongeza siku Tatu za kuandikisha Wananchi katika Daftari la Wapiga kura kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.
Uamuzi huo wa Serikali umetangazwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo, ambapo kwa sasa uandikishaji huo utafanyika hadi Oktoba 17 badala ya Oktoba 14 kama ilivyotangazwa hapo awali.
