Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt Ayub Rioba, amewataka Vijana nchini kuenzi na kuziishi fikra za Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kuwa amani iliyopo nchini inatokana na mapenzi yake kwa Tanzania.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kumbukumbu ya miaka Ishirini ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere linalofanyika mkoani Lindi, Dkt Rioba amesema kuwa, Vijana lazima wajivunie uongozi wa Mwalimu Nyerere kwani ndio uliojenga misingi ya amani iliyopo hapa nchini.
“Vijana lazima mjivunie amani iliyopo hapa nchini, kwani bila hivyo sasa hivi mngekua porini mnapigana vita, ila Mwalimu alijenga amani ya Taifa hili kutokana na mapenzi yake kwa Tanzania”, amesema Dkt Rioba.
Ameongeza kuwa Vijana lazima wailinde amani ya Taifa ili kuenzi mambo mema aliyoaacha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa Watanzania.
