Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amejiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu.
Waziri Mkuu Majaliwa na Mke wake Mary Majaliwa, wamejiandikisha katika kituo cha Shule ya Msingi ya Nandagala wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Zoezi za uandikishaji Wananchi katika Daftari la Wapiga Kura kwa ajili ya uchaguzi huo lilianza tarehe Nane mwezi huu na litakamilika Jumatatu tarehe 14.
