Rais Magufuli amemaliza ziara yake mkoani Katavi baada ya kuzindua miradi mbalimbali na kuzungumza na Wakazi wa mkoa huo katika mikutano ya hadhara.
Tayari Rais Magufuli ameondoka mkoani Katavi kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), ambayo imeanza safari yake ya kwanza hii leo kutoka mkoani Dar es salaam kwenda mkoani Katavi.
Rais Magufuli na ujumbe wake amesafiri kwa kutumia ndege hiyo muda mfupi baada ya kuzindua safari hiyo ya kwanza.
Kwa takribani siku Tisa, Rais Magufuli amekua na ziara katika mikao mitatu, ziara iliyoanzia mkoani Songwe, baadaye kuelekea mkoani Rukwa na amemaliza ziara yake katika mkoa huo wa Katavi.
