Rais John Magufuli amewataka Wakimbizi kutoka nchini Burundi waliopo nchini hasa wilayani Tanganyika mkoani Katavi, kuheshimu sheria za nchi wawapo hapa nchini.
Amesema kuwa, kama Wakimbizi hao wameamua kuendelea kuishi hapa nchini basi waache vitendo viovu vinginevyo warejee nchini mwao.
https://www.youtube.com/watch?v=kQ3n4uMbhPI&feature=youtu.be
Rais Magufuli ameyasema hayo mkoani Katavi, wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Majarida wilayani Tanganyika, ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo.
Amesema kuwa Wakimbizi hao walikimbia machafuko nchini mwao, lakini kwa sasa amani imerejea nchini Burundi, hivyo wanaweza kurejea nchini humo badala ya kufanya vitendo hivyo viovu hapa nchini.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa, Tanzania haiwafukuzi nchini Wakimbizi hao bali wakati umefika kwa wao kurejea nchini mwao na kuendeleza Taifa lao.
Amesema kuwa Tanzania ni nchi ya amani, na kamwe haitawavumilia Raia kutoka nje kuvuruga amani hiyo.
