Waziri Lugola ashauri kuwepo kwa kodi ya mdomo

0
241

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ametoa wito kwa Watanzania kuacha kusema mambo mabaya kuhusu Rais John Magufuli na kuacha kubeza jitihaza zake mbalimbali zenye lengo la kuwaletea maendeleo.

Waziri Lugola ametoa wito huo wakati wa ziara ya Rais Magufuli mkoani Katavi na kumshauri Rais kwa kuwa yeye ndio anayeridhia kodi mbalimbali, aridhie kuwepo kwa kodi ya matumizi mabaya ya mdomo endapo vitendo vya kumbeza vitaendelea.