Azma ya kuifanya Dodoma ya kijani iko pale pale

0
207

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, azma ya Serikali yakuifanya Dodoma kuwa ya kijani iko pale pale.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo baada ya kutembelea shamba la miti
lililopo katika eneo la Mzakwe jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya
ufuatiliaji wa kampeni aliyozindua mwaka 2017.

Ameupongeza uongozi wa Kambi ya Jeshi la Makutupora, Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Watendaji wa Ofisi yake kwa kuhakikisha miti hiyo iliyopandwa mwezi Disemba mwaka 2017 inastawi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kambi ya Jeshi ya Makutupora Luteni Kanali
Festo Mbaga amesema kuwa, miti 2,976 sawa na asilimia 90.3 ya miti 2, 300 iliyopandwa katika shamba hilo imestawi.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza TFS kukamilisha tafiti za sampuli ya udongo iliyochukuliwa ili kubaini aina ya miti inayostawi katika jiji la Dodoma.