Mwalimu Mkuu aachiwa huru kwa mara ya pili

0
196

Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Kigoma, imemwachilia huru kwa mara nyingine Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyantore katika Halmashauri ya wilaya ya Kigoma, -Jason Rwekaza, aliyeachiliwa huru kwa mara ya kwanza Septemba 16 mwaka huu na kukamatwa tena Septemba 19 kwa tuhuma Tatu za kumdhalilisha na kumpa Ujauzito Mwanafunzi wake.

Rwekaza ameachiwa huru baada ya upande wa Serikali kusema kuwa, hauna nia ya kuendelea na shitaka hilo.

Hakimu Elia Baha wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Kigoma amesema kuwa, amemwachia huru Mwalimu Mkuu Rwekaza chini ya kifungu cha 91 kifungu kidogo cha kwanza cha mwenendo wa makosa ya jinai.