YouTube kuwasaidia Wagombea kunadi sera zao

0
945

Mtandao wa YouTube umeanzisha kifaa maalum kinachojulikana kama Instant Reserve, ambacho kinaweza kutumiwa na Wagombea wa maeneo mbalimbali kunadi sera zao kwa wapiga kura.

Kupitia mtandao huo, Wanasiasa wanaweza kutumia vizuri majukwaa ya mtandaoni kujinadi kwa sera zao ili kuwafikia watu wengi zaidi na kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kimataifa, kifaa hicho kitawawezesha Wanasiasa kupanga mbinu zitakazoendesha kampeni zao na kuwapa nafasi ya kunadi sera zao kupitia mtandao huo wa You Tube.