Taasisi za Umma zatakiwa kuitumia Mamlaka ya Serikali Mtandao

0
168

Serikali imepiga marufuku Taasisi za umma kutumia fedha kuzilipa Taasisi binafsi ili kupatiwa huduma ambazo pia zinazotolewa na Mamlaka ya Serikali Mtandao.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Ruvuma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika, wakati akizungumza na Watumishi wa Umma wilayani Namtumbo.

Waziri Mkuchika yuko mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi, kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani humo.