Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kesho itatoa utabiri wa mvua za msimu mrefu kuanzia mwezi Novemba mwaka huu hadi Aprili mwaka 2019 kwa mikoa inayopata msimu mmoja wa mvua.
Mikoa hiyo ni pamoja na Lindi, Mtwara, Iringa, Njombe, Rukwa, Mbeya, Dodoma, Singida na Tabora.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi amesema kuwa, lengo la kutoa utabiri huo ni kuwawezesha Waka zi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari ya madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa mvua hizo.
