Serikali ya Uturuki imetangaza kuwa, muda wowote kuanzia sasa vikosi vyake vitaanza mashambulio ya kujihami katika mpaka wa nchi hiyo na Syria, ili kuzuia mashambulio kutoka kwa Waasi.
Uturuki imesema haitafanya mashambulio hayo peke yake, bali itakuwa ikisaidiana na Wapiganaji wanaoiunga mkono Serikali ya nchi hiyo.
Uturuki ilitangaza kupeleka vikosi vyake nchini Syria baada ya Marekani kutangaza kuwa inaondoa Majeshi yake nchini humo.
