Serikali kuendelea kujenga miundombinu

0
198

Rais John Magufuli amesema kuwa, Serikali itaendelea kujenga miundombinu katika maeneo mbalimbali nchini, kwa kuwa fedha za kufanya hivyo zipo.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo mkoani Katavi wakati wa uzinduzi wa barabara ya Kanazi – Kizi – Kibaoni yenye urefu wa Kilomita 76.6, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Amesema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha nchi inakua na miundombinu ya uhakika hasa barabara, ambazo zitayaunganisha maeneo yote nchini.

Rais Magufuli ameongeza kuwa, kwa sasa Serikali ina pesa za kutosha zikiwemo zile zinazorejeshwa na Watuhumiwa wa makosa ya Uhujumu Uchumi waliokiri makosa yao na kuomba kusamehewa, hivyo moja ya kazi za fedha hizo ni kujenga miundombinu katika maeneo mbalimbali nchini.