Rwanda yazindua Smartphone

0
1047

Kampuni ya Mara ya nchini Rwanda imezindua simu mbili za kisasa (Smartphones), na kuwa nchi ya kwanza kutengeneza aina hiyo ya simu Barani Afrika.

Hatua ya Rwanda ya kuzindua simu hizo za kisasa inadhihirisha maono ya nchi hiyo kujiimarisha katika masuala ya Teknolojia.

Simu hizo ambazo zimepewa majina ya Mar X na Mara Z, zitatumia mfumo wa Google wa Android na zinatarajiwa kuuzwa kuanzia Dola 130 hadi Dola 190 za Kimarekani.

Inaelezwa kuwa simu hizo zilizozinduliwa nchini Rwanda, zinatarajiwa kushindana na simu za kampuni ya Samsung, ambazo simu zake ni za bei nafuu zaidi kwani kuanza kuuzwa kuanzia Dola 54 za Kimarekani.

Akizindua simu hizo, Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema kuwa, ni matumaini yake kuwa simu za aina hiyo zitaongeza matumizi ya simu aina ya Smartphone miongoni mwa Raia wa Rwanda ambapo kwa takwimu za hivi karibuni, watumiaji wa simu nchini humo ni asilimia 15 tu.