Tanzania yapata mkopo wa zaidi ya Shilingi Trilioni Moja

0
245

Benki ya Dunia imeipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa Dola 450 za Kimarekani ambazo ni sawa na zaidi ya Shilingi Trilioni Moja, kwa ajili ya mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) awamu ya Tatu.

Makubaliano ya kuipatia Tanzania mkopo huo yamesainiwa jijini Dar es salaam kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Bella Bird.

James amesema kuwa, Benki ya Dunia imeipatia Tanzania mkopo huo wa masharti nafuu baada ya kuridhishwa na mafanikio ya utekelezaji wa TASAF awamu ya Kwanza na ya Pili, ambapo Kaya masikini zilisaidiwa ili ziweze kujiongezea kipato na kumudu gharama mbalimbali muhimu za kijamii.