SUMA JKT yakabidhi jengo la Madini

0
234

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amekabidhiwa jengo la umahiri la Madini kutoka Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) mkoani Mara, ambalo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia Mia Moja.

Akipokea jengo hilo Naibu Waziri Nyongo amesema kuwa, mbali na kutumika kwa shughuli za Madini, pia litatumika kama kituo cha kutoa elimu kwa Wachimbaji Wadogo wa migodi, ikiwemo ile ya uchorongaji Madini na Ujasiriamali.

Naibu Waziri huyo wa Madini amelipongeza Shirika hilo la SUMA JKT kwa kufanya kazi nzuri na kuwataka kufanya hivyo katika miradi mingine.