Mapigano Tripoli yasababisha kukosekana kwa huduma muhimu

0
902

Mapigano katika Mji Mkuu wa Libya, -Tripoli ambayo yamedumu kwa muda wa miezi Sita, yamesababisha mji huo kuwa na tatizo la kukosekana kwa huduma za maji, mafuta pamoja na umeme.

Habari Zaidi kutoka mjini Tripoli zinaeleza kuwa, mapigano hayo pia yamesababisha kuenea kwa uchafu katika mji huo ambao hapo awali ulikua na sifa ya usafi.

Mji huo wa Tripoli umekua katika mapigano ambayo yamekua yakifanywa na vikosi vya Serikali pamoja na vile vinavyomuunga mkono mbabe wa Kivita Jenerali Khalifa Haftar.