Kamati ya maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeushauri uongozi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kufanya tafiti za kina wakati wa kuandaa vipindi na kuandaa habari ili maudhui yake yawe bora.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Joseph Mapunda amesema hayo jijini Dar es salaam, wakati walipokutana na Menejimenti ya TBC kwa lengo la kujionea utendaji kazi wa Shirika hilo, kuona mafanikio na changamoto zilizopo ili kuzitafutia ufumbuzi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBC, – Martha Swai amewaeleza Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa, Shirika hilo limekua likijitahidi kutimiza majukumu yake kwa kuzingatia misingi ya utamaduni wa Taifa.
Kamati hiyo ya maudhui ya TCRA pia imetembelea maeneo mbalimbali ya TBC, ikiwemo gari la kurushia matangazo ya moja kwa moja na studio za kurushia matangazo ya Televisheni.
