Aliyesababisha kukatika kwa umeme asimamishwa kazi

0
161

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amemsimamisha kazi kiongozi aliyekuwa zamu katika kituo cha kupooza umeme wa gridi ya Taifa Ubungo jijini Dar es salaam, kwa tuhuma za uzembe uliosababisha kukatika kwa umeme usiku wa kuamkia hii leo katika jiji la Dar es salaam na Zanzibar.

Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa ziara yake katika kituo hicho, Waziri Kalemani amesema kuwa tatizo la kukatika umeme kutokana na uzembe ni lazima lipatiwe ufumbuzi haraka iwezekanavyo.