Marekani yaonywa kuhusu mpango wake wa kuongeza ushuru

0
3662

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema kuwa, Marekani ijiandae kuwekewa vikwazo na nchi za Umoja wa Ulaya, endapo itaendelea na mpango wake wa kuziwekea nchi hizo ushuru mpya wa bidhaa.

Marekani imetangaza kuwa itaweka ushuru wenye thamani ya Dola Bilioni 7.5 za Kimarekani kwa bidhaa kutoka katika nchi hizo zinazoingia Marekani.

Bidhaa ambazo Marekani imepanga kuongeza ushuru kutoka katika Umoja wa nchi za Ulaya, ni bidhaa za mvinyo na jibini.

China ndiyo ilikuwa nchi ya kwanza kwa bidhaa zake kuongezewa ushuru nchini Marekani,  hali iliyosababisha mgogoro wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.