Rais Buhari wa Nigeria aanza ziara Afrika Kusini

0
944

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria yuko nchini Afrika Kusini kwa ziara ya kikazi,  ikiwa ni ziara ya kwanza kwa kiongozi huyo nchini humo tangu Nigeria ilipowarejesha nyumbani Raia wake Mia Sita waliokuwa wakiishi nchini humo.

Buhari amesema kuwa, pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, kuhusu mustakabali wa Raia wa Nigeria wanaofanyabiashara nchini Afrika Kusini.

Nigeria ililazimika kuwarejesha Raia wake nyumbani, baada ya kushambuliwa, kuuawa na wengine rasilimali zao kuchomwa moto kutokana na chuki dhidi ya wageni iliyozuka nchini Afrika Kusini.