Tusiruhusu mfumo mpya katika ununuzi wa Korosho : Waziri Mkuu

0
193

 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza Wakuu wa mikoa yote nchini inayolima korosho, kuhakikisha wanasimamia vizuri zao hilo na wasiruhusu kuingizwa kwa mfumo mpya wa ununuzi ambao haujaeleweka kwa Wadau na Wanunuzi.
 

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo mkoani Mtwara, alipokua akizungumza na Wakazi wa mkoa huo baada ya kukagua ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini inayojengwa katika eneo la Mitengo.

Amesema msimu wa korosho kwa mwaka huu unatarajiwa kutangazwa hivi karibuni, hivyo ni lazima Wakuu wa mikoa inayolima korosho wakajiandaa vizuri ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.

“Mabadiliko  ya mifumo yalitolewa na baadhi ya Viongozi ambao sio waaminifu, Serikali iko macho itawachukulia hatua viongozi wa vyama vya ushirika wasiokuwa waaminifu, tunataka mfumo wenye manufaa ndio utumike”, amesisitiza Waziri Mkuu Majaliwa.
 
Amewataka Wafanyabiashara kutojihusisha na ununuzi wa korosho kwa njia ya kangomba na kwamba watakaojihusisha watachukuliwa hatua za kisheria.