Moto wazuka tena katika misitu ya Amazon

0
983

Kumekuwa na matukio ya kuzuka tena kwa moto katika misitu ya Amazoni nchini Brazil, misitu inayotegemewa na mataifa mengi katika nchi za Amerika ya Kusini baada ya moto wa awali kudhibitiwa.

Habari zinasema kuwa, kwa siku Sita mfululizo katika baadhi ya maeneo ya msitu wa Amazoni umezuka moto mwingine kwenye maeneo tofauti, ingawa habari zinasema moto huo umedhibitiwa katika kipindi hiki ambapo maeneo mengi ya msitu huo ni makavu.

Asilimia Thelathini ya eneo la misitu wa Amazoni hivi sasa ni kavu, hali inayofanya moto kuwaka kwa kasi, huku pia upepo mkali katika eneo hilo ukiongeza nguvu ya moto huo kuwaka.