Nyota wa Tenesi nchini Uingereza, – Andy Murray, ametinga hatua ya Tatu ya mashindano ya wazi ya Tenesi ya China baada ya kumbwaga Muingereza mwenzake Cameron Norrie kwenye mchezo wa hatua ya Pili kwa ushindi wa seti mbili kwa moja za 7-6, 7-6 na 6-1.
Huo unakuwa mwanzo mzuri kwa Murray ambaye amewahi kukamata nafasi ya kwanza kwa ubora nchini Uingereza na mshindi mara Tatu wa mataji makubwa (Grand Slams), lakini akiwa na mwendo wa kusuasua kwenye mashindano ya karibuni aliyoshiriki.
Kuboronga huko ni kwenye mashindano hayo, ikiwemo kuondoshwa kwenye hatua ya kwanza ya mashindano ya Cincinnati Masters na mashindano ya wazi ya Winston Salem, matokeo yaliyomfanya nyota huyo kuporomoka hadi kwenye nafasi ya 513 kwenye viwango vya ubora wa mchezo huo Duniani.