Ufafanuzi wa Ikulu kuhusu uteuzi

0
169

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imetoa ufafanuzi kuhusu uteuzi uliofanywa hivi karibuni, ambapo aliyehamishwa kituo cha kazi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida ni John Magalula.

Uhamisho huo umefanywa na Rais John Magufuli hii leo.

Aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es salaam ni Charangwa Makwiro na uteuzi wake umefanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika, naye ni kuanzia hii leo.