Kesi ya Kabendera yahairishwa

0
145

Kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili Mwandishi wa Habari, – Erick Kabendera imeahirishwa hadi tarehe 11 mwezi huu itakapotajwa tena.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo jijini Dar es salaam kuwa, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika katika maeneo kadhaa.