Zaidi wa watu 500 waliofichwa Nigeria wapatikana

0
1060

Polisi nchini Nigeria wamewaokoa zaidi ya watu Mia Tano, waliokua wamefichwa katika nyumba moja kwenye mji wa Kaduna.

Watu hao ambao wote ni Wanaume, inadaiwa walichukuliwa mateka na kufichwa ndani ya nyumba hiyo, na wamekua wakipatiwa mateso makali na kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji.

Mkuu wa Polisi katika mji huo wa Kaduna, – Ali Janga amesema kuwa, baada ya kuvamia nyumba hiyo wamekuta watu hao wote wamefungwa minyororo kama Watumwa.

Amesema kuwa, waliamua kuvamia nyumba hiyo baada ya Wakazi wa eneo hilo kutoa taarifa polisi kuwa, wana wasiwasi na shughuli zinazoendelea ndani ya nyumba hiyo.

Watu Wanane wanashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Nigeria kufuatia tukio hilo, japo mpaka sasa haijafahakika watu waliokua wakiwashikilia watu hao mateka walikua na lengo gani.

Mateka wengine waliookolewa ni watoto wa kiume, ambao wamewaeleza polisi kuwa walipelekwa kwenye nyumba hiyo na ndugu zao, ambao walidhahani kuwa nyumba hiyo ni shule ya Quran.