Watanzania wametakiwa kuzungumza mambo mema ya nchi yao

0
307

Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania – KKKT, Usharika wa Kijitonyama Dkt Eliona Kimaro ameelezea umuhimu wa Watanzania kuzungumza habari njema kuhusu Taifa, ikiwemo miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Katika mahubiri yake hii leo wakati wa Ibada ya asubuhi jijini Dar es salaam, Dkt Kimaro amesema kuwa Rais John Magufuli ni matokeo ya maombi ya Watanzania, waliotaka kupata kiongozi atakayewatumikia na kuongoza
mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa ambavyo vinadidimiza maisha ya Wanyonge.

Ameongeza kuwa, wanaosema Serikali
imebana, hakuna fedha, wajitafakari huku akionesha kuwashangaa
wanaosambaza habari mbaya kuhusu Tanzania.

Amesema Watanzania hawapaswi kulalamika kuwa serikali haijafanya kitu, kwani kazi inafanyika kila mahali na inaonekana.

Kiongozi huyo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania – KKKT, Usharika wa Kijitonyama Dkt Eliona Kimaro amewataka Watanzania kujenga tabia ya kuzungumza mema kuhusu nchi yao, na kuwatia moyo viongozi ambao wamejitoa
kuwatumikia.